Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 13:25

Wakimbizi wakumbwa na Njaa Nigeria


Wakimbizi wakingoja msaada wa chakula katika moja wapo ya kambi za wakimbizi katika Jimbo la Borno Nigeria.
Wakimbizi wakingoja msaada wa chakula katika moja wapo ya kambi za wakimbizi katika Jimbo la Borno Nigeria.

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wa kutoa msaada kwa kibanadamu wameripoti hali ya ukosefu wa lishe pamoja na kiangazi kwenye jimbo la Borno la Nigeria.

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wa kutoa msaada kwa kibanadamu wameripoti hali ya ukosefu wa lishe pamoja na kiangazi kwenye jimbo la Borno la Nigeria ambako wanamgambo wa Boko Haram wamefanya hali ya kilimo kuwa ngumu.

Shirika la masuala ya kibinadamu linasema mapigano katika eneo hilo yamefanya shughuli ya kupeleka misaada kwenye kambi za wakimbizi kuwa ngumu. Ofisi ya Umoja wa mataifa inayoratibu maswala ya kibinadamu (OCHA) imesema watu 275,000 wanaishi kwenye kambi 15.

Nigeria ilitangaza dharura ya ukosefu wa chakula katika Jimbo la Borno mwezi aliopita na kupelekea Umoja wa Mataifa kutuma msaada wa dola milioni 13.

Mapigano dhidi ya kundi la Boko Haram yamekuwa yakiendelea kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu 2009 ambapo zaidi ya watu 20,000 wameuwawa na wengine milioni2.7 kukoseshwa makazi.

XS
SM
MD
LG