Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:51

Ni miaka 10 toka Tsunami itokee


Wakazi wa Aceh, nchini Indonesia wakisoma dua kwenye kaburi la halaiki la waliokufa katika maafa ya Tsunami, wakiadhimisha miaka kumi toka Tsunami itokee. Maahimisho yamefanyika Ijumaa tarehe 26, mwaka 2014.
Wakazi wa Aceh, nchini Indonesia wakisoma dua kwenye kaburi la halaiki la waliokufa katika maafa ya Tsunami, wakiadhimisha miaka kumi toka Tsunami itokee. Maahimisho yamefanyika Ijumaa tarehe 26, mwaka 2014.

Maombolezo katika fukwe, muda wa kukaa kimya na sala zimefanyika barani Asia, Ijumaa kuadhimisha miaka kumi ya kimbunga katika bahari ya Hindi cha Tsunami, ambacho kiliua watu wanaokadiriwa kuwa 220,000 mwaka 2004.

Wimbi kubwa lilikumba darzeni ya nchi zilizo katika mwambao wa bahari ya Hindi, barani Asia na Afrika.

Tsunami iliharibu kabisa jamii za mwambao, kumaliza familia na kushambulia fukwe zilizojaa watalii asubuhi baada ya sikukuu ya Krismas.

Maafa hayo yalisababishwa na tetemeko la ardhi baharini lenye kipimo cha rikta 9.1 na kutengeneza wimbi lenge nguvu zaidi kwa kipindi cha miaka 40 lililokuwa na mwendo kasi wa ndege, na kwenda mpaka pwani ya Afrika Mashariki.

Tsunami ilikuwa na nguvu kubwa na kusababisha mstari wa dunia kutikisika kwa sentimeta chache.

Moja ya eneo lililoshambuliwa zaidi ni jimbo la Indonesia, Aceh ambapo maadhimisho yalifanyika Ijumaa.

Makamu wa Rais wa Indonesia, Jusuf Kalla, amekumbuka namna ulimwengu ulivyojumuika pamoja kufuatia maafa hayo.

XS
SM
MD
LG