Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:10

Dunia yakaribisha 2016


Fataki za kukaribisha mwaka mpya mjini Bangkok, Thailand, Jan. 1, 2016.
Fataki za kukaribisha mwaka mpya mjini Bangkok, Thailand, Jan. 1, 2016.

Huku kukiwa na tahadhari za usalama miji mbali mbali duniani ilifanya sherehe za kukaribisha mwaka mpya wa 2016 kwa maonyesho ya fataki, muziki na kila namna ya shamra shamra.

Katika jiji la New York ambako kwa kawaida kunakuwa na sherehe kubwa za mwaka mpya hapa Marekani maelfu kwa maelfu ya watu walijazana katika eneo la Times Square kushuhudia sherehe za kukaribisha mwaka mpya.

Usalama ulikuwa mkali katika eneo hilo katikati ya Manhattan huku kukiwa na mamia ya polisi na watu wakikaguliwa kabla ya kuingia katika eneo la sherehe.

Salamu za mwaka mpya 2016
Salamu za mwaka mpya 2016

Miji kadha mikubwa barani Afrika kama vile Dar es salaam, Tanzania, Nairobi, Kenya, Johannesburg na mingineyo Afrika Magharibi ilikaribisha mwaka mpya saa kadha kabla ya nchi za Ulaya na Marekani.

Nchi za Asia, katika miji kama Sydney, Australia na Bangkok, Thailand, zilikuwa za kwanza kukaribisha mwaka mpya wa 2016 kwa maonyesho mazuri ya fataki

Mjini Dubai watu walikaribisha mwaka mpya kwa maonyesho makubwa ya fataki wakati huo huo moto ukiwa unawaka katika hoteli moja maarufu katikati ya mji huo - Address Hotel - ambayo ilishika moto katika ghorofa ya 20 saa kadha kabla ya mwaka mpya kuingia.

Maafisa wa mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, waliamua kufuta sherehe rasmi za kukaribisha mwaka mpya kwa hofu ya vitendo vya kigaidi. Brussels ni mji ambako walitokea magaidi waliotekeleza shambulizi la kigaidi la mjini Paris, Ufaransa, mwaka jana.

XS
SM
MD
LG