Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:49

IGAD yaunga mkono hatua ya Kenya dhidi ya al-Shabab


Wanajeshi wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Afrika katika kitongoji cha Mogadishu
Wanajeshi wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Afrika katika kitongoji cha Mogadishu

Jumuiya ya IGAD ilifikia uamuzi huo katika mkutano wa ngazi ya mawaziri mwishoni mwa wiki

Nchi sita za Afrika Mashariki wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya IGAD zimeahidi kuipa Kenya uungaji mkono kikamilifu katika hatua zake za kijeshi dhidi ya kundi la al-Shabab kusini mwa Somalia. Baadhi ya nchi katika jumuiya hiyo zinatafakari kuisaidia Kenya kijeshi katika juhudi hizo huku al-Shabab ikionyesha dalili ya kupoteza udhibiti wa eneo hilo.

Jumuiya ya IGAD ilifanya mkutano maalum wa mawaziri wa nchi hizo Ijumaa mjini Addis Ababa, siku tano baada ya Kenya kuvamia maeneo ya al-Shababa nchini Somalia. Zaidi ya vikosi viwili vya Kenya vikishirikiana na majeshi ya anga vimeingia kusini mwa Somalia baada ya al-Shabab kushutumiwa kwa mfululizo wa utekaji nyara wa watalii na wafanyakazi wa misaada ndani ya Kenya.

Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo mjini Addis Ababa ilisema IGAD inafurahishwa na hatua za Kenya kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Huku kukiwa na ripoti kuwa majeshi ya Kenya yanakaribia mji muhimu wa bandari unaoshikiliwa na al-Shabab, Kismayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Moses Wetangula ametoa wito wa msaada wa kimataifa katika kumalizi udhibiti wa al-Shabab nchini Somalia.

XS
SM
MD
LG