Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:52

NATO yafunga shughuli za kijeshi Afghanistan


Bendi ya majeshi ya ushirika ikitumbuiza wakati wa ushushwaji wa Bendera Kabul kumaliza miaka 13 ya shughuli za kijeshi za NATO Desemba 8, 2014.
Bendi ya majeshi ya ushirika ikitumbuiza wakati wa ushushwaji wa Bendera Kabul kumaliza miaka 13 ya shughuli za kijeshi za NATO Desemba 8, 2014.

NATO imeshusha bendera yake ya shughuli za kijeshi nchini Afghanistan Jumatano wakati umoja huo wa kijeshi unamiliza miaka 13 ya kupambana na Taliban na Al-Qaida.

Marekani iliongoza uvamizi wa majeshi ya ushirika Afghanistan Oktoba 2001 kuondoa utawala wa Taliban ambao ulikuwa ukishirikiana na wanamgambo wa Al-Qaida waliohusika na mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Marekani mwezi mmoja kabla.

Lakini wakati NATO inaondoa shughuli zake za msaada wa ulinzi katika mapambano, kundi la Taliban linaendeleza mashambulizi nchini kote.

Shambulio la kijeshi katika kituo cha polisi jimboni Kandahar Jumatatu limesababisha vifo vya karibu watu watano. Shambulio hilo lilifuatia mfululizo wa mashambulizi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kabul.

Jenerali wa Marekani John Campbell amesema Jumatatu kwamba vikosi vya Afghanstan vimeongeza uimara katika kulinda nchi yao.

Marekani itawaacha askari wake karibu 11,000 Afghanistan hata baada ya mwaka 2014. Baadhi ya nchi katika ushirika huo wa NATO nazo zitaacha baadhi ya vikosi pia.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka shirika la habari la Associate Press (AP), karibu askari wa nje 3,500 wameuwawa nchini Afghanistan tangu kuingia nchini humo mwaka 2001, wengi wao wakiwa ni Wamarekani.

Idadi ya waliokufa miongoni mwa vikosi vya Afghanistan imekuwa kubwa mno ikiwa ni karibu na askari 10,000 waliouawa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita peke yake.

XS
SM
MD
LG