Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:42

Nape:CCM haishtushwi kuhama kwa makada wake, kitashinda


Dr. John Magufuli mgombea kiti cha rais wa CCM
Dr. John Magufuli mgombea kiti cha rais wa CCM

Chama tawala nchini Tanzania-CCM kilisema hakishtushwi na wimbi la baadhi ya makada wake maarufu wanaokihama chama hicho kwenda vyama vingine vya upinzani wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar Es Salaam, Jumatatu na katibu wa NEC itikadi na uenezi katika chama cha CCM, bwana Nape Nnauye katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini humo ikiwa ni kauli ya mwanzo kutolewa na kiongozi wa juu wa chama hicho tangu aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa zamani nchini Tanzania bwana Edward Lowassa kuamua kukihama chama tawala na kwenda chama cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA huku akifuatiwa na makada wengine akiwemo Naibu Waziri wa kazi na ajira Dr. Makongoro Mahanga aliyetangaza kukihama chama hicho siku ya Jumapili.

Nape alisema chama cha CCM bado kinauhakika mkubwa wa kushinda licha ya kuwepo na ushindani huo mkubwa katika uchaguzi wa mwaka huu kutokana na wimbi hilo la kuhama kwa baadhi ya makada wake.

Mgombea urais wa CCM John Magufuli
Mgombea urais wa CCM John Magufuli

Chama tawala cha CCM kilizungumzia pia kura za maoni za udiwani na ubunge kupitia chama hicho zilizofanyika nchini kote Jumamosi ambapo kuliripotiwa matumizi makubwa ya fedha huku baadhi ya viongozi waandamizi serikalini wakishindwa kupita katika kura hizo za maoni.

​Wakati huo huo chama cha CCM kilitangaza kwamba mgombea wake wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu Dr. John Magufuli anatarajiwa kuchukua fomu za kugombea kiti hicho kwenye ofisi ya tume ya taifa ya uchaguzi siku ya Jumanne huko jijini Dar Es Salaam.

wagombea wengine wa vyama vya upinzani ambao tayari wameshachukua fomukatika tume ya taifa ya uchaguzi ni kutoka vyama vya UPDP, TLP, DP na CHAMA CHA UKOMBOZI WA UMMA.


XS
SM
MD
LG