Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:54

Mzozo wa kisiasa waongezeka Libya


Wingu la moshi laonekana baada ya ndege za kivita kushambulia eneo la Misrata mjini Tripoli Agosti 23, 2014
Wingu la moshi laonekana baada ya ndege za kivita kushambulia eneo la Misrata mjini Tripoli Agosti 23, 2014

Libya imekumbwa na mzozo wa kisiasa tangu kutimuliwa madarakani kwa diktekta Moammar Gadhafi mwaka 2011

Mzozo wa kisiasa na kijeshi uliongezeka Libya Jumatatu baada ya chama mseto cha kiislam kinachodhibiti mji mkuu wa Tripoli kumteuwa waziri mkuu mpya na kutangaza kuwa limefutilia mbali bunge jipya.Waziri mkuu Abdullah al Thani alijibu kwa kuyaita makundi ya wapiganaji wa kiislam,wadhalimu na kusisitiza kuwa hawawezi kutawala nchi hiyo kwa nguvu.

Waziri mkuu mpya aliyeteuliwa tena majuzi Abdullah al-Thani aliwaambia waandishi habari katika mji wa Tobruk ulioko mashariki mwa nchi kuwa wanamgambo wa kundi la Fajr walioteka nyara uwanja wa ndege wa Tripoli Jumamosi wanajaribu kushinikiza ajenda zao kwa nguvu na kwamba hatua zake za kisiasa ni kinyume cha sharia.

Wakati huo,huo Marekani na washirika wanne wa mataifa makubwa ya Ulaya wameonya mataifa ya nje dhidi ya kuingilia kati mzozo wa Libya.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani pamoja na Uingereza, Ufaransa,Ujerumani na Italy, walitoa taarifa Jumatatu ikisema hatua za watu wa nje zinaongeza migawanyiko nchini Libya na zinadumaza demokrasia.

Washirika hao watano wanalaani mapigano katika miji mikubwa kama Tripoli na Benghazi na kwenye maeneo ya makazi na wanavisihi vyama vyote kukubali kusitisha mapigano na kuungana pamoja kuunda serikali ya mpito.

Libya imekumbwa na mzozo wa kisiasa tangu kutimuliwa madarakani kwa diktekta Moammar Gadhafi mwaka 2011.

XS
SM
MD
LG