Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 02:25

Mvutano unachelewesha kuidhinishwa waziri mkuu Somalia


Rais Sharif Sheik Ahmed, kulia, akizungumza bungeni katika kikao cha kwanza cha bunge tangu kuteua waziri mkuu mpya, Mohamed Abdullahi Mohamed. Spika wa bunge Sherif Hassan Sheik Adan, amesimama upande wa kushoto.
Rais Sharif Sheik Ahmed, kulia, akizungumza bungeni katika kikao cha kwanza cha bunge tangu kuteua waziri mkuu mpya, Mohamed Abdullahi Mohamed. Spika wa bunge Sherif Hassan Sheik Adan, amesimama upande wa kushoto.

Rais Sheik Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia, anasema ni lazima kwa wabunge kupiga kura kwa njia ya wazi, huku spika wa bunge Sharif Hassan Shiekh Aden anasema bunge litapiga kura kwa siri kuidhinisha uteuzi wa waziri mkuu mpya.

Hali hiyo ya kutoelewana imezusha mvutano mpya wa kisiasa na kuchelewesha kuidhinisha uteuzi wa Mohamed Abdullahi Mohamed. Hata hivyo mbunge Abdullahi Shiek akizungumza na Sauti ya Amerika Jumapili amesema, majadiliano yanefanyika kutanzua mvutano huo kati ya rais na spika wa bunge.

Bw Sheik anasema sababu ya kuahirishwa kwa kikao cha bunge ni kuruhusu muda zaidi wa mashauriano kati ya wabunge ili kuhakikisha kura ya kuidhinisha uteuzi wa waziri mkuu unafanyika kufuatana na sheria.

Siku ya Jumapili Rais Sharif alitoa wito kwa spika, kwa maneno yake kuheshimu sheria na kutowazuia wabunge kutekeleza wajibu wao wa kikatiba.

Mbunge Shiek anasema, mvutano huu ni sehemu ya utaratibu wa kuunda upya demokrasia huko Somalia. Serikali ya mpito ya Somalia imekua ikikumbwa na mivutano kati ya wajumbe wake kwa muda sasa na kuwa kizingiti kikubwa cha kuendelea mbele na kuweza kuwashinda wanaharakati wa kislamu nchini humo.

Baadhi ya wachambuzi wanasema ugomvi huo unapeleka ujumbe mbaya kwa Jumuia ya Kimataifa na Wasomali na huwenda ukawapatia nguvu zaidi waasi wenye siasa kali kuongeza mashambulizi yao dhidi ya utawala wa Mogadishu.

XS
SM
MD
LG