Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:22

Rais Sata wa Zambia aruhusiwa kuingia Malawi


Rais wa Zambia Michael Sata(R) akila kiapo cha kuongoza nchi huko Lusaka, Zambia. Ijumaa Septemba 23, 2011
Rais wa Zambia Michael Sata(R) akila kiapo cha kuongoza nchi huko Lusaka, Zambia. Ijumaa Septemba 23, 2011

Serikali ya Malawi imemruhusu Rais mpya wa Zambia Michael Sata kuingia tena nchini humu baada ya kufukuzwa nchini humo

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika anasema serikali yake itamruhusu Rais mpya aliyechaguliwa nchini Zambia kuingia nchini humo, miaka minne baada ya kusafirishwa kwa nguvu chini ya mipango isiyofahamika.

Serikali ya bwana Mutharika ilieleza Alhamis kwamba Rais Michael Sata ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa Zambia wiki iliyopita ameondolewa marufuku zote za uhamiaji dhidi yake tangu alipochaguliwa kuwa mkuu wa taifa.

Mwaka 2007, maafisa wa usalama nchini Malawi walimkamata Bwana Sata wakati akiwa kwenye safari yake binafsi katika mji mkuu wa kibiashara wa Blantyre. Maafisa kisha walimsafirisha maili kadhaa kuelekea mpaka wa Zambia kabla ya kumshusha na kumuwekea marufuku ya kuingia nchini humo.

Maafisa wa usalama wa Malawi hawajawahi kusema bayana kwa nini bwana Sata alifukuzwa nchini humo. Taarifa ya bwana Mutharika ya Alhamisi ilisema kufukuzwa huko kulitokana na “matukio maalum”.

Bwana Sata ameishitaki serikali ya Malawi kuhusu suala hilo lakini kesi bado ipo mahakamani.

Uhusiano kati ya Malawi na Zambia umekuwa mzuri kihistoria tangu uhuru wao kutoka kwa Uingereza katika miaka ya 1960.

XS
SM
MD
LG