Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:25

Mkenya aweka rekodi mpya ya marathon


Moses Mosop, kushoto , na Geoffrey Mutai walikuwa bega kwa bega huku ikiwa imebakia maili moja katika Boston Marathon, Aprili, 18 2011
Moses Mosop, kushoto , na Geoffrey Mutai walikuwa bega kwa bega huku ikiwa imebakia maili moja katika Boston Marathon, Aprili, 18 2011

Mkenya Geoffrey Mutai ashinda mbio ndefu za Boston marathon kwa rekodi mpya ya dunia.

Mwanariadha wa kenya Geoffrey Mutai ameweka rekodi mpya ya dunia katika mbio ndefu za marathon kwa kushinda mbio za Boston marathon Jumatatu katika muda wa saa mbili, dakika tatu na sekunde 02. Naye Caroline Kilel wa Kenya pia alishinda upande wa wanawake katika muda wa saa mbili, dakika 22 na sekunde 36.

Wakenya kwa jumla walitawala mbio hizo. Kwa upande wa wanaume Moses Mosop alichukua nafasi ya pili katika muda wa saa 2, dakika 3 na sekunde 06 akifuatiwa na Gebregziabher Gebremariam wa Ethiopia katika muda wa saa 2, dakika 4 na sekunde 53. Robert Kiprono Cheruiyot na Philip Kimutai Sanga wote wa Kenya walimaliza katika nafasi za sita na saba.

Caroline Kilel
Caroline Kilel

Kinadada wa Kenya nao pia walitawala mbio za wanawake. Kufuatia ushindi wa Caroline, nafasi ya pili ilichukuliwa na Mmarekani Desiree Davila aliyemaliza katika muda wa saa 2, dakika 22 na sekunde 38. nafasi ya tatu ilikwenda kwa Sharon Cherop aliyemaliza katika muda wa saa 2, dakika 22 na sekunde 42 na Mkenya mwingine Caroline Rotich alichukua nafasi ya nne katika muda wa saa 2, dakika 24 na sekunde 52. Alice Timbili alimaliza katika nafasi tisa.

XS
SM
MD
LG