Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:25

Museveni ataka wapinzani wamuombe radhi


Rais wa Uganda Yoweri Museveni (L) akiwa na mpinzani wake wa kisiasa Kizza Besigye mjini Kampala
Rais wa Uganda Yoweri Museveni (L) akiwa na mpinzani wake wa kisiasa Kizza Besigye mjini Kampala
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewataka viongozi wawili waandamizi wa upinzani nchini Uganda kuacha mapambao ya kisiasa wasiyoweza kushinda na badala yake wajiunge na chama tawala cha National Resistance Movement-NRM.

Bwana Museveni alimshutumu mpinzani wake Kizza Besigye na meya wa Kampala, Erias Lukwago kwa kupinga program za maendeleo za serikali na kutangaza uongo. Alitaka aombwe msamaha na wapinzani hao wawili.

Lakini wote Besigye na Lukwago walipuuza wito wa Museveni wakiuita mchezo wa kisiasa wa kutaka kupata uungaji mkono wa chama tawala katika mji mkuu ambako wapiga kura mara nyingi hawakiungi mkono chama tawala.

Rais Museveni na chama chake tawala cha NRM wamekuwa madarakani tangu mwaka 1986. Lakini Lukwago anasema matamshi ya karibuni ya Museveni ni matokeo ya kile anachosema kinaonekana ni mgawanyiko katika chama tawala.

Lukwago alisema maafisa wa utawala mara kwa mara wanakataa kufanya kazi na wapinzani kuhusu wasi wasi wa umma shutuma ambazo wawakilishi wa chama tawala wanazikanusha hazina ukweli. Wanaushutumu upinzani kwa kuzorotesha juhudi za serikali za kuendeleza sheria na kanuni na kuhakikisha amani na uthabiti nchini humo. Kitu ambacho Lukwago hakubaliani nacho.
XS
SM
MD
LG