Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:28

Mugesera arejeshwa Rwanda kutoka Canada


Leon Mugusera (kushoto), pamoja na mkewe (kati) na binti yake (kulia), wakitoka nje ya mahakama April 12, 2001 mjini Quebec City.
Leon Mugusera (kushoto), pamoja na mkewe (kati) na binti yake (kulia), wakitoka nje ya mahakama April 12, 2001 mjini Quebec City.

Serikali ya Rwanda imethibitisha kurejeshwa kwake ambapo anashukiwa kuhusika kwenye mauaji ya mwaka 94 alipokuwa naibu mwenyekiti wa kilichokuwa chama tawala cha MRND

Zaidi ya muongo mmoja akipinga kurejeshwa Rwanda, mmoja wa washukiwa wakuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda Bwana Leon Mugesera, anarejeshwa nchini humo hii leo akitokea Canada ambako amekuwa akiishi kwa karibu miongo miwili..

Bwana Leon Mugesera ambaye mpaka leo anachukuliwa Rwanda kama mmoja wa watu waliokuwa na siasa kali za kibaguzi na ambaye alichochea waziwazi mauaji ya kimbari hatimaye juhudi zake za kupinga kurejeshwa Rwanda zimegonga mwamba.

Kwa miaka sasa kumekuwepo na vuta nikivute baina ya ngazi za sheria za Rwanda na Canada kufuatia madai ya Mugesera ya kukataa kurejeshwa Rwanda kwa madai kwamba anaweza kuuawa au kuteswa akiwa kizuizini.

Hatua hii ilisababisha tume ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu kuingilia kati hapo awali na kuzuia asiletwe lakini baadaye mahakama nchni Canada zikaamua kuwa madai yake hayana msingi.

Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ya Rwanda Bwana Martin Ngoga awali alisema kuwa Rwanda haitesi mahabusu na madai hayo hayana msingi wowote.

"Tumekuwa tukifuatilia kesi hii kwa miaka kumi na tisa sasa na tunadhani muda unatosha kwa ngazi zozote za sheria kufanya maamuzi kama haya. Sisi si serikali inayotesa washukiwa na tunadhani hata wanasheria wa Canada wanalitambua hilo na ndiyo maana wameamua kumrejesha hapa"

Lakini madai ya mshukiwa huyo ambaye amekuwa akilalamika kuwa akiletwa Rwanda anaweza kufanyiwa unyama yanapewa umuhimu gani na watetezi wa haki za binadamu?

Juhudi za kutaka kuzungumza na maafisa wa tume ya kutetea haki za binadamu nchini hapa hazikuwezekana lakini kwa njia ya simu mmoja wa makamishina wakuu wa tume hiyo Bwana Laurent Nkongoli anasema,

"Sioni sababu ya yeye kuwa na wasiwasi juu ya maisha yake kwa sababu sisi kama watetezi wa haki za binadamu tupo hapa na mimi binafsi nimekuwa nikifuatilia haki zao, ninachoweza kusema Rwanda imeweka saini makubaliano ya kimataifa yanayopambana na vitendo vya unyanyasaji,tunawatembelea mahabusu na kuhakikisha wanapata haki zao za msingi, nadhani huo ni wasiwasi wake tu lakini hakuna tatizo".

Bwana Leon Mugesera mwenye umri wa miaka 59 aliyekuwa naibu mwenyekiti wa chama tawala kwenye serikali ya Juvenali Habyarimana anashukiwa kuhamasisha wahutu kufanya mauaji dhidi ya watutsi ambao yeye aliwaita mende walioingia kutoka nchi za kigeni, akisema watauawa kisha wasafirishwe kupitia mto Nyabarongo hadi kwao Abyssinia…

XS
SM
MD
LG