Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:38

Mswada wa mashoga wawasilishwa tena bungeni Uganda


Mwanamke mmoja akibeba bango wakati wa maandamano kupinga tabia ya mapenzi ya watu wa jinsia moja mjini Jinja Uganda.
Mwanamke mmoja akibeba bango wakati wa maandamano kupinga tabia ya mapenzi ya watu wa jinsia moja mjini Jinja Uganda.

Mswada dhidi ya wapenzi wa jinsia moja umewasilishwa bungeni Jumanne kwa mara nyingine tena.

Mswada huu uliwasilishwa bungeni mara ya kwanza mwaka wa 2009 kwenye bunge la nane ambalo muhula wake ulimalizika mwaka jana.

Kulingana na sheria za bunge, ikiwa mswada huu ungejadiliwa tena, ilibidi uwasilishwe tena kwenye bunge la tisa.

Mbunge Ndorwa, David Bahati, ndiye aliuwasilisha mswada huu ambao ulipingwa sana na wafadhili miaka miwili iliyopita.

Kwa wakati mmoja wafadhili mkiwemo Sweden walitishia kukomesha kuipa msaada serikali ya Uganda ikiwa mswada huu utapitishwa.

Kwenye kikao cha kwanza cha bunge mwaka huu, miongoni mwa masuala yaliyopewa kipa umbele ni mswada dhidi ya mashoga.

Mbunge David Bahati alimuomba spika wa bunge Rebecca Kadaga na bunge limkubalie mswada dhidi ya mashoga usomwe kwa mara ya kwanza akisema kuwa unalenga kuhifadhi maadili ya Waganda.

Miongoni mwa mapendekezo ya mswada huu ni hukumu ya kifo kwa shoga atakayemlazimisha kijana ambaye hajaufikisha umri wa miaka kumi na minane kushiriki katika ngono au akimwambukiza mtu ugonjwa wa ukimwi.

Wengine watakaoadhibiwa na mswada huu ni watu watakaoshiriki kwenye vitendo ambavyo vinaonekana kama vinaupigia dembe ushoga. Vitendo hivi vyaweza kuwa kuchapisha makala yanayousifia ushoga, kuzitetea haki za mashoga au kuwafadhili kwa njia yoyote ile.

Mswada huu uliwasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza mwaka wa elfu mbili na tisa. Serikali za nchi za magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu waliukashifu vikali wakisema ni mswada unaokadamiza haki za mashoga za kushiriki ngono na mtu watakaye.

XS
SM
MD
LG