Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:17

Morsi kufikishwa mahakamani leo


Mtu akimbeba mtoto wanakimbia kutokana na gesi ya tukowa machozi wakati wa mapambano kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa rais wa zamani Mohamed Morsi mjini Cairo, Jan. 17, 2014.
Mtu akimbeba mtoto wanakimbia kutokana na gesi ya tukowa machozi wakati wa mapambano kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa rais wa zamani Mohamed Morsi mjini Cairo, Jan. 17, 2014.
Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani jumanne ikiwa ni moja ya mashtaka ya uhalifu yanayomkabili kiongozi wa chama cha kiislamu.

Bwana Morsi na zaidi ya wanachama 100 wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood wanakabiliwa na mashtaka kwa kutoroka jela mwaka 2011 na shutuma za kuua polisi wakati wa mapinduzi ambayo yamemuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Rais Hosni Mubarak na kumuingiza madarakani bwana Morsi.

Washtakiwa wengi wametambuliwa kuwa ni wanachama wa kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hamas, kundi la wanamgambo la Hezbollah lenye makao yake nchini Lebanon na kikosi cha Revolutionary Guard cha Iran.

Morsi na wafuasi wake wakiwa mahakamani Nov. 4, 2013
Morsi na wafuasi wake wakiwa mahakamani Nov. 4, 2013
Bwana Morsi na wanachama wengine waandamizi wa kundi la Brotherhood pia wanakabiliwa na mashtaka kwa shutuma za kuchochea mauaji ya waandamanaji wa upizani wakati akiwa madarakani.

Rais huyo wa zamani na watu wengine 35 pia watashtakiwa kwa shutuma za upelelezi kwa kushirikiana na kundi la wapalestina la Hamas.

Jeshi la Misri lilimuondoa mamlakani bwana Morsi mwezi July mwaka jana. Hosni Mubarak aliondolewa madarakani kufuatia upinzani wa umma ambao ulianza Januari mwaka 2011.
XS
SM
MD
LG