Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:56

Moi aipinga rasimu ya katiba mpya


Ramani ya Kenya.
Ramani ya Kenya.

Rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi amekuwa mstari wa mbele kupinga rasimu ya katiba mpya. Rais huyo mstaafu anadai kuwa rasimu hii ya katiba ni mawazo ya kigeni.

Rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi amekuwa mstari wa mbele kupinga rasimu ya katiba mpya. Rais huyo mstaafu anadai kuwa rasimu hii ya katiba ni mawazo ya kigeni.

Bwana Moi anasema atazunguka pembe zote za nchi ya Kenya kuwahimiza wapiga kura kukataa rasimu hii ya katiba. Amewashutumu vikali wanasiasa wanaodai kwamba watu kutoka mkoa wa Rift Valley watatengwa na serikali kwa sababu wanapinga rasimu hii ya katiba.

Rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi.
Rais mstaafu wa Kenya Daniel Arap Moi.

Wakati huo huo kampeni kali zimeanza nchini Kenya kuunga mkono au kupinga rasimu ya katiba mpya huku tume ya uchaguzi nchini humo ikiwa imetangaza alama maalumu zitakazotumiwa wakati wa kura ya maoni kuhusu katiba mpya.
Muda mfupi baada ya tume kutangaza tarehe ya kura hiyo ya maoni wanasiasa na watu mbali mbali wameanza kampeni kali za kuunga mkono au kupinga rasimu hii ya katiba. Tume hiyo ya uchaguzi nchini humo pia imetangaza alama au nembo maalumu zitakazotumiwa na pande zote mbili wakati wa kura ya maoni.

Upande wa serikali ukiongozwa na Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga, utatumia alama ya rangi nyekundu. Upande wa upinzani ukiongozwa na viongozi wa makanisa ya kikristo watatumia rangi ya kijani kibichi. Tayari Rais Kibaki, Makamu Rais Kalonzo Musyoka, na Waziri Mkuu Odinga wamehutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika bustani mashuhuri ya Uhuru Park ya mjini Nairobi.

Nao wanasiasa wengine wanaopinga rasimu hii ya katiba wameanza kuzunguka katika sehemu za mashambani nchini humo kuwahimiza wapiga kura kupinga suala hili.

XS
SM
MD
LG