Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:59

Trump amchagua mpinzani wa mabadiliko ya hali ya hewa kuongoza idara ya mazingira


 Scott Pruitt, mwanasheria mkuu wa Oklahoma, akiwasili kukutana na rais mteule Donald Trump katika jengo la Trump Tower, New York City, Dec. 7, 2016.
Scott Pruitt, mwanasheria mkuu wa Oklahoma, akiwasili kukutana na rais mteule Donald Trump katika jengo la Trump Tower, New York City, Dec. 7, 2016.

Chaguo la Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, kuongoza idara ya mipango ya mazingira EPA inazusha malalamiko makubwa kutoka wapinzani na watetezi wa mazingira na kua ni tishio kuu wa hatua zote muhimu za kukabiliana na hali ya hewa na uchafuzi wa mazingira zilziochukuliwa na utawala wa Rais Barack Obama.

Mwanasheria Mkuu wa jimbo la Oklahoma ni mmoja wa maafisa kutoka majimbo 27 ambao walifungua mashtaka hapo Januari kutaka mpango wa nishati salama uzuiliwe, ambao kupitia EPA ilitaka majimbo kutayarisha mipango mbadala ya kuzuia uchafuzi wa mazingira kwa asilimia 32 chini kidogo ya viwango vya mwaka 2005 ifikapo mwaka 2030. Na wakati huo huo kuongeza kiwango cha uzalishaji wa nishati mbadala.

Seneta wa Montana, Steve Daines amesema anaridhia juhudi za Pruitts katika kupinga mpango mzima wa mazingira wa Obama.

“Ninatarajia kuona akipangua mpango mzima wa nishati salama kipengere baada ya kipengere kama kiongozi wa EPA,” aliongeza Daines.

Seneta wa Oklahoma James Inhofe amempongeza Pruitt kama kiongozi wa masuala ya mazingira.

“Pruitt amendelea kupinga ukiukwaji wa katiba na kanuni za kupindukia za mazingira, kama vile Maji ya Marekani na Mpango wa Nishati Salama; amethibitisha kuwa usimamizi mzuri wa mazingira haumaanishi kuwabebesha mzigo mkubwa walipa kodi na wafanyabiashara kupitia ukiritimba,” alisema Inhofe katika taarifa yake.

Makamu rais wa zamani Al Gore awasili kukutana na Donald Trump
Makamu rais wa zamani Al Gore awasili kukutana na Donald Trump

Trump amewashangaza wengi alipomtangaza Pruitt kua mkuu wa EPA idara ambayo amekua akiikosowa vikali na hasa baada ya kukutana na mtetezi mkuu wa mazingira makamu rais wa zamani Al Gore na msani Leonardo DiCaprio siku moja kabla.

Mwezi Februari Mahakama kuu ilitoa amri ya kusitisha utekelezaji wa kanuni hizo wakati upinzani wa kisheria ukiendelea. Ilirudisha kesi hiyo hadi mahakama ya kukata rufaa ya Washington, kutathminiwa upya.

Mabadiliko ya Hali ya Hewa

Pruitt ameeleza mashaka yake kuhusu ukweli wa mabadiliko ya hali ya hewa. Yeye na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Luther Strange wameandika katika jarida la National review mwezi Mei wakikosoa majimbo ambayo yanachukua hatua za kisheria dhidi ya makampuni ambayo yamekaidi sayansi au dhana ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Trump ametoa kauli zinazo tofautiana kuhusu madaliko ya hali ya hewa katika miaka ya karibuni akisema kuwa ni mzaha, lakini aliiambia New York Times mwezi uliopita kuwa kuna “kuna uhusiano fulani” na matendo ya wanadamu.

“Inategemea kwa kiwango gani. Inategemea pia ni ukubwa gani wa gharama zitazikabili kampuni zetu,” Trump alisema.

Gharama ni sehemu ya hoja inayotolewa na majimbo katika kesi dhidi ya Idara ya Kuhifadhi Mazingira (EPA). Wanadai malengo ya Obama katika kuzuia uchafuzi wa mazingira hayawezi kufikiwa kwa kufanya mabadiliko katika viwanda vilivyopo vinavyozalisha nishati inayosababisha uchafuzi.

XS
SM
MD
LG