Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:16

Uganda yashinda dhahabu ya kwanza katika mbio za nyika


Vijana chini ya miaka 20 katika mbiyo za nyika mjini Kampala 2017
Vijana chini ya miaka 20 katika mbiyo za nyika mjini Kampala 2017

Jacob Kiplimo ameipatia Uganda nishani yake ya kwanza ya dhahabu katika mbio za nyika duniani mjini Kampala, Uganda siku ya Jumapili, alipoibuka mshindi katika mashindano ya vijana chini ya miaka 20.

Kiplimo akishangiliwa na maelfu ya Waganda alipofanikiwa kuwabwaga wanariadha hodari kutoka Kenya na Ethiopia.

Muda mfupi baadae timu ya Ethiopia ilishinda nishani yake ya kwanza ya dhahabu katika mbio za wasichana chini ya miaka 20 pale Letesenbet Gidey alipowashinda Wakenya Hellen Lobun na Celliphine Chespo kwa kutumia dakika 18 sekunde 13.

Kenya imekuwa nchi ya kwanza kushinda nishani ya dhahabu katika mashindano hayo ya 2017, pale bingwa wa dunia na Olympiki Asbel Kiprop alipowaongoza Wakenya wengine Winfred Nzisa, Beatrice Chepkoech na Bernard Koros kutwaa dhahabu wakitumia dakika 22 sekunde 22.

Timu ya Kenya ya mchanganyiko Asbel Kiprop, Beatrice Chepkoech, Winnie Mbithe and Bernard Koros
Timu ya Kenya ya mchanganyiko Asbel Kiprop, Beatrice Chepkoech, Winnie Mbithe and Bernard Koros

Hiyo ilikuwa ni mashindano ya kwanza ya mchanganyiko wanaume na wanawake ya kupokezana vijiti kuandaliwa na Shirikisho la Riadha Duniani IAAF katika mbiyo za nyika.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na IAAF yamerejea Afrika Mashariki baada ya miaka Kumi.

Kabla ya Uganda kukabidhiwa fursa ya kuwa mwenyeji mwaka huu, Kenya iliandaa mashindano hayo katika mji wa Mombasa mwaka wa 2007.

XS
SM
MD
LG