Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 00:35

Korea Kaskazini yawafukuza waandishi wa BBC


Kim Jong Un
Kim Jong Un

Jinsi Korea Kaskazini inavyowatendea wanahabari wa kimataifa inadumaza taswira iliyokarabatiwa vyema na serikali ya Kim Jong Un inayowasilishwa katika mkutano wa chama unaoendelea mjini Pyongyang.

Korea Kaskazini iliwafukuza wanahabari wa BBC leo Jumatatu, inaonekana kwasababu maafisa wa serikali hawakupendezwa na ripoti zao. Rupert Wingfield-Hayes, ambaye ni mwandishi wa BBC mjini Tokyo, pamoja na mzalishaji Maria Byrne na mpiga picha Matthew Goddard, walizuiliwa siku ya Ijumaa wakati wakiwa karibu kuondoka nchini humo.

Wingfield-Hayes alihojiwa kwa muda wa saa nane. Wanahabari hao wa BBC walikuwa Korea Kaskazini kabla ya mkutano wa Workers Party Congress wakifuatana na ujumbe wa tuzo ya Nobel ambao walikuwa wanafanya utafiti.

XS
SM
MD
LG