Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:55

Kampuni ya Mitsubishi yashutumiwa kwa kutoa habari isiyo sahihi


MITSUBISHI MOTORS LOGO
MITSUBISHI MOTORS LOGO

Kampuni ya Mitsubishi Motors iko mashakani kufuatia shutuma kwamba wafanyakazi wake wamekuwa wakifanya udanganyifu na kudai kwamba magari yake yanatumia kiasi kidogo cha petroli kuliko inavyostahiki.

Siku ya Alhamisi, maafisa wa uchukuzi katika serikali ya Japan wamevamia afisi za kampunmi ya Mitsubishi Motors mjini Tokyo, kufuatia kukiri kwa kampuni hiyo kwamba ilifanya ulaghai kwenye majaribio ya kupima jinsi magari yake elfu mia sita yanavyotumia kiasi kidogo cha petroli.

Shirika la habatri la AFP liliripoti kwamba maafisa walivamia kituo cha utafiti cha kampuni mwendo wa asubuhi na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kampuni hiyo kutozwa faini ya kiwango cha juu kuhusiana na kashfa hiyo.

Afisa wa ngazi za juu katika serikali ya Japan, YOSHIHIDE SHUGA, aliwaambia wanahabari kwmaba serikali inalipa umuhimu mkubwa swala hilo kwani haitaki wananchi wake na wateja wengine kufanyiwa ulaghai.

"Hii imeathiri pakubwa Imani waliyonayo wateja wa kampuni hii, na hili ni swala tunalolipa umuhimu mkubwa," alisema.

Kufuatia kashfa hiyo, bei ya hisa za kampuni hiyo kwenye soko la hisa la Tokyo zilionekana kushuka kwa asili mia ishirini, huku kampuni hiyo ikitangaza kwamba itasitisha utengenezaji na uuzaji wa magari madogo aina ya Mini, na kuongeza kwamba idadi ya magari yaliyo kwenye orodha yenye utata, huenda ikaongezeka kwa kiasi kikubwa.

Kashfa hii inafuatia nyingine iliyogunduliwa septemba mwaka jana ambayo ilihusu magari ya kampuni ya Volkswagen kuhusika katika uchafuzi wa mazingira.

XS
SM
MD
LG