Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 08:18

Misri: Pande zote zajichimbia


Maelfu na maelfu ya wa Misri wanaompina Rais Hosni Mubarak wamekusanyika kwenye uwanja wa Tahrir, Cairo wakimba nyimbo za kumtaka rais wao aondoke madarakani.
Maelfu na maelfu ya wa Misri wanaompina Rais Hosni Mubarak wamekusanyika kwenye uwanja wa Tahrir, Cairo wakimba nyimbo za kumtaka rais wao aondoke madarakani.

Waandamanaji waliendelea kumiminika katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo Jumatano, wakati wengine wakienea katika maeneo mengine na huku watu zaidi wakijiunga na maandamano hayo.

Ridhaa zinazotolewa na serikali inaelekea hazijatosha kutuliza joto au kuleta dalili za kumalizika kwa mgogoro huo.

Baadhi ya waandamanaji wameondoka katika uwanja wa Tahrir na kuingia maeneo mengine mbele ya bunge la Misri. Wameapa kuendelea na upinzani huo mpaka Rais Hosni Mubarak na serikali yake wajiuluzu.

Hali kadhalika, makundi mapya yanajiunga katika upinzani huo. Wafanyakazi wa viwandani na serikali wameanza kujitokeza kudai nyongeza ya mishahara.

Na baadhi ya vyama vya wafanyakazi navyo pia vinajiunga, huku wafanyakazi wanachama wakigoma katika maeneo mengine ya nchi, kutokea Helwan, kusini mwa Cairo, mpaka Suez.

Madai ya waandamanaji wa kisiasa yamebaki yale yale: mageuzi katika mfumo wa serikali yakiambatana na mageuzi ya kweli ya katiba na kumalizika kwa hali ya dharura ambayo imeruhusu serikali kukamata watu hovyo, kuwekwa ndani bila kesi na utesaji wa watuhumiwa kwa karibu miaka 30.

XS
SM
MD
LG