Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:16

Milipuko yazuka tena Ivory Coast


Mwanajeshi wa serikali ya Ivory Coast akitayarisha silaha yake mjini Abidjan Ivory Coast, April 14, 2011
Mwanajeshi wa serikali ya Ivory Coast akitayarisha silaha yake mjini Abidjan Ivory Coast, April 14, 2011

Mashahidi wanasema milipuka na milio ya bunduki kubwa kubwa ilisikika katika eneo moja la mji wa Abdijan na kusababisha wakazi kutafuta usalama kwingineko.

Mapigano mapya yamelipuka mjini Abdijan leo Jumatano huku majeshi ya rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara yakishambulia wapiganaji wanaomtii kiongozi aliyeondolewa madarakani Laurent Gbagbo.

Mashahidi wanasema milipuko na milio ya bunduki kubwa kubwa ilisikika katika eneo la Yopougon, nje kidogo ya Abdijan, na kusababisha wakazi wengi kukimbia kutafuta usalama kwingineko.

Serikali mpya ya Ouattara inajaribu kurejesha hali ya ushwari baada ya miezi minne ya ghasia za kisiasa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Maafisa wametoa wito wa utulivu lakini makundi ya wanamgambo yanaendelea kumwunga mkono Gbagbo ambaye alitiwa nguvuni na majeshi ya Ouattara wiki iliyopita, baada ya majeshi ya Ufaransa na Umoja wa Mataifa kushambulia makazi yake.

XS
SM
MD
LG