Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 14:52

24 wauwawa kwa mlipuko nchini Afghanistan


Maafisa wa polisi wa Afghanistan
Maafisa wa polisi wa Afghanistan

Milipuko tofauti ya bomu nchini Afghanistan hii leo imeuwa watu wasiopungua 24 na kuwajeruhi kiasi cha 40 wengine.

Shambulizi hilo lililosababisha vifo lilitokea mjini Kabul wakati mjitoa mhanga alipokaribia kwenye basi dogo akiwa kwa miguu na kuwasha milipuko.

Wizara ya mambo ya ndani nchini Afghanistan inasema shambulizi hilo limesababisha vifo vya watu 14 na wanane kujeruhiwa.

Kundi la Taliban haraka lilidai kuwajibika.

Watu waliouwawa walikuwa walinzi wa usalama kutoka Nepal wakifanya kazi kwenye kampuni moja ya kigeni katika mji mkuu wa Afghanistan. Rais watano wa Nepal waliokuwa ndani ya basi pia walijeruhiwa pamoja na raia wane wa Afghanistan.

Saa chache baadae, bomu lililotegwa barabarani na waasi lililipuka katika sehemu nyingine ya mji ambapo mjumbe mmoja wa halmashauri katika jimbo alijeruhiwa pamoja na walinzi wake wawili.

Mkurugenzi mkuu wa Afghanistan, Abdullah Abdullah, amelaani shambulizi kama kitendo cha ugaidi na uchochezi.

XS
SM
MD
LG