Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:16

Michele Obama ashangiliwa kwa hotuba yake DNC


First lady Michelle Obama, speaking at the Democratic National Convention in Philadelphia, Pa., tells the audience, 'Don't let anyone ever tell you that this country isn't great.' (A. Shaker/VOA)
First lady Michelle Obama, speaking at the Democratic National Convention in Philadelphia, Pa., tells the audience, 'Don't let anyone ever tell you that this country isn't great.' (A. Shaker/VOA)

Mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama, alishangiliwa kwa muda mrefu alipotoa hotuba yake katika mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Demokratik cha hapa Marekani, ulioanzaJumatatu katika mji wa Philadelphia, jimbo la Pennsylvania. Bi Obama ni mmoja wa viongozi wa ngazi za juu waliozungumza katika siku ya kwanza ya kongamano hilo.

Ukumbi wa Mkutano mkuu wa DNC
Ukumbi wa Mkutano mkuu wa DNC

Mke huyo wa rais anayeondoka alianza hotuba yake kwa kuzungumzia umuhimu wa wanasiasa kuyajali masilahi ya watoto wanapofikiria kuhusu sera na wakati wanatoa matamshi hadharani, na kusema kuwa mgombea urais mteule wa chama hicho, Bi Hillary Clinton, ana wasifu wa kutosha na uzoefu unaohitajika kuwa rais wa Marekani.

"Kwa kila neno tunalolitamka, na kila hatua tunayoichukua, ni vyema kukumbuka kwamba watoto wetu wanatutazama kwa makini," aliemba Bi Obama.

"Kuna mtu mmoja tu ambaye ninaamini anahitimu kuwa rais wa Marekani. Na huyo mtu ni rafiki yetu Hillary Clinton," aliongeza.

Mkutano huo ulifunguliwa huku Chama hicho kikijaribu kuonyesha kuwa wanachama wake pamoja na wafuasi wa Seneta Bernie Sanders wana umoja baada ya kashfa kuhusu barua pepe zilizotolewa kwa siri na kuchapishwa na tovuti ya wikileaks, zilizoonyesha kuwa viongozi wa chama cha Demokratik, walimpendelea bi Hillary Clinton dhidi ya mpinzani wake katika uchaguzi wa awali, Bernie Sanders.

Bernie Sanders akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa chama cha Demokratic
Bernie Sanders akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa chama cha Demokratic

Meya wa mji wa Baltimore, jimbo la Maryland, STEPHANIE RAWLINGS BLAKE, ambye pia ndiye katibu wa kamati ya kitaifa ya chama hicho, aliufungua mkutano huojana Jumatatu, akichukua nafasi ya DEBBIE WASSERMAN SHULTZ, ambaye ni mwenyekiti anayeondoka wa chama hicho.

Wasserman Shultz alilazimika kujiuzulu kutoka kwa wadhifa huo siku ya Jumapili baada ya mtandao wa Wikileaks kufichua yaliyokuwemo katika barua pepe elfu ishirini.

Mke wa rais Barack Obama akiwa miongoni mwa wazungumzaji wsakuu leo amewahimiza wanachama kumpigia kura Hillary Clinton na katika kitendo cha nadra kwa mke wa rais kushambulia mgombea wa upinzani namna alivyofanya bila ya kumtaja Bw Trump kwa jina.

Wafusi wa NBernie Sander ndani ya ukumbi wa mkutano mkuu wa Demokratic
Wafusi wa NBernie Sander ndani ya ukumbi wa mkutano mkuu wa Demokratic

Kabla ya mkutano huo kuanza, Sanders aliwarai wafuasi wake kumuunga mkonio bi Clinton. Hata hivyo, baadhi ya waliokuwa kwenye ukumbi walimpigia makelele ya kuashiria kutofurahishwa na kauli yake aklipowataka wampigie kura Clinton.

Waliotoa hotuba ni pamoja na Seneta wa jimbo la Massachusetts, Elizabeth Warren, na seneta wa jimbo la New Jersey, Cory Booker.

XS
SM
MD
LG