Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:45

Miaka mitano sasa toka tetemeko la Haiti


Picha za wakati na baada ya tetemeko laardhi la nchini Haiti.
Picha za wakati na baada ya tetemeko laardhi la nchini Haiti.

Nchi ya Haiti Jumatatu ya Desemba 12, 2015, inaadhimisha miaka mitano toka kutokea kwa tukio baya la tetemeko la ardhi.

Likiwa na nguvu za 7.0 kwenye kipimo cha rikta , tetemeko la Januari 12, mwaka 2010 liliua zaidi ya watu 200,000.

Zaidi ya watu milioni moja waliachwa bila makazi, na kulazimishwa kuishi katika vituo vya mahema vilivyo tengenezwa kwa maboksi ama plastiki.

Ugonjwa wa kipindupindu ulizuka punde baada ya tetemeko hilo la ardhi, na kuleta tatizo lingine katika nchi hiyo ya kikaribian ambayo ndiyo masikini kuliko zote katika ukanda wa magharibi wa pembe ya dunia.

Mpaka Jumatatu baadhi ya sehemu zilizo athirika katika mji mkuu wa Port-au-Prince, zimebadilika sana na vifusi vimeondolewa kutoka maeneo mengi ya mji huo.

Hata hivyo pamoja na juhudi mbali mbali ya kukabiliana na tetemeko zilizofanywa bado maelfu ya watu wanaendelea kuishia katika hali ngumu ya kimaisha.

XS
SM
MD
LG