Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:45

Mgogoro wa Misri katika wiki ya pili


Mwanamke wa Misri akiangalia umati wa waandamanaji kutokea nyumbani kwake Cairo.
Mwanamke wa Misri akiangalia umati wa waandamanaji kutokea nyumbani kwake Cairo.

Maelfu ya waandamanaji Ijumaa walijazana tena katika Uwanja wa Tahrir wakibeba mabango na bendera za Msiri wakitaka Rais Hosni Mubarak ajiuzulu mara moja.Mgogoro huo unakaribia kumaliza wiki ya pili bila dalili ya kumalizika haraka.

Waandamanaji hao waliisema Ijumaa ndiyo 'siku ya kuondoka' kwa Mubarak ingawaje Rais huyo alisema katika hotuba aliyotoa mapema wiki hii kuwa ataendelea kukaa madarakani mpaka muhula wake utakapomalizika Septemba mwaka huu.

Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kutoka Cairo, Ismail Mfaume, mhadhiri wa chuo kikuu cha Al Ahzar nchini Misri, alisema Rais Mubarak haelekei kutingishwa na maandamano ya raia wake wenye hasira. Badala yake amezijibu nchi za magharibi zinazomtaka aondoke madarakani akisema kuondoka kwake kutaiweka Misri katika hatari zaidi ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood kutwaa madaraka. Mfaume anasema nchi za magharibi zina wasiwasi juu ya kundi hilo ambalo linaungwa mkono na Iran, Hamas na kundi la Hezbollah la Lebanon.

XS
SM
MD
LG