Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 08:02

Mfanyakazi wa UN afariki kwa Ebola


Wafanyakazi wa afya wakiwa wamevalia nguo za kujikingfa na maambukizo ya Ebola
Wafanyakazi wa afya wakiwa wamevalia nguo za kujikingfa na maambukizo ya Ebola

Shirika la afya duniani –WHO, limesema vifo kutokana na ugonjwa wa Ebola vimepanda na kufikia watu 4,447 huku visa vya idadi ya walioambukizwa ikikaribia elfu tisa.

Siku ya Jumanne, naibu mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bruce Aylward alisema idadi ya visa vipya vilivyo ripotiwa imefikia 8,914.

Shirika la habari la kimataifa la Reuters limemnukukuu akisema kuwa akisema kwamba visa hivyo vinatarajiwa kufika 9,000 mwishoni mwa wiki.

Awali siku ya Jumanne mfanyakazi wa umoja wa mataifa alieambukizwa akihudumia wagonjwa Liberia alifariki katika hospitali moja ya Ujerumani.

Ripoti kutoka hospitali hiyo ya St George ilioko Leipzig zinasema mgonjwa huyo aliyekuwa na umri wa miaka 56 alifariki usiku wa Jumanne licha ya kupewa matibabu maalum.

XS
SM
MD
LG