Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:29

Mfanyakazi wa ndani Uganda ahukumiwa miaka minne


Mtumishi wa nyumbani Tumuhiirwe akimkanyaka mtoto mdogo Kampala
Mtumishi wa nyumbani Tumuhiirwe akimkanyaka mtoto mdogo Kampala

Kesi hiyo imefuatiliwa kwa ukaribu katika nchi za Afrika Mashariki na dunia nzima baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Tumuhiirwe, akimpiga na kumkanyaga mtoto huyo.

Mahakama nchini Uganda imemuweka hatiani na kutoa hukumu ya kifungo cha miaka mine gerezani mfanyakazi wa ndani Jolly Tumuhiirwe, kwa kumtesa mtoto wa miezi nane.

Mfanyakazi huyo mwenye miaka 22 alikubali kutenda makosa wiki iliyopita mahakamani ya kumtesa mtoto aliyekuwa anamuhudumia.

Kesi hiyo imefuatiliwa kwa ukaribu katika nchi za Afrika Mashariki baada ya video kusambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Tumuhiirwe, akimpiga na kumkanyaga mtoto huyo.

Mwanasheria wa mfanyakazi huyo wa ndani Ladislaus Rwakafuuzi, Jumatatu alisema hukumu hiyo ni stahiki na hana matarajio ya kukata rufaa huku akisema mahakama imewasemea waganda wengi.

Tumuhiirwe alisema mahakamani kwamba alisukumwa kutenda ukatili huo kutokana na kutotendewa haki na muajiri wake ambaye ni mzazi wa mtoto aliyemtesa.

Hata hivyo msichana huyo aliwaomba radhi wazazi wa mtoto na umma kwa ujumla na kudai hakujua nini kilimtokea hadi kutenda ukatili huo.

Kesi hiyo imetoa mwito kwa maofisa wanaohusika na ustawi wa watoto kutaka wanaofanya kazi na watoto wapewe mafunzo na kuthibitishwa ili kuajiriwa.

XS
SM
MD
LG