Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:27

Mdahalo wa Makamu Rais wakamilika Marekani


Makamu Rais Joe Biden (L) na Paul Ryan wa chama cha Republican katika mdahalo wa wagombea Makamu Rais 2012, Marekani
Makamu Rais Joe Biden (L) na Paul Ryan wa chama cha Republican katika mdahalo wa wagombea Makamu Rais 2012, Marekani
Mdahalo wa kusisimua wa wagombea wenza wa kiti cha makamu rais Marekani, kati ya makamu rais Joe Biden wa chama cha Democratic na mbunge wa Wisconsin, Paul Ryan wa chama cha Republican umemalizika Alhamis ambapo kila mmoja alitetea vikali sera za vyama vyao kuhusiana na masuala ya ndani na kigeni pamoja na huduma za jamii.

Mdahalo ulianza kwa suala la shambulio la mwezi uliyopita dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani huko Benghazi nchini Libya. Makamu Rais, Biden alisema hilo lilikuwa ni jambo la kusikitisha mno akiahidi kwamba makosa yaliyofanyika wakati huo hayatofanyika tena. Biden alimtetea Rais kwamba hakujuwa kwamba ubalozi mdogo wa Marekani huko Libya ulihitaji ulinzi zaidi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Akiulizwa kwanini serikali inabadilisha jinsi mambo yalivyotokea huko Libya alisema “ jamii ya ujasusi iliwaarifu mambo hayo walipokuwa wanapata habari zaidi na walibadilisha muelekeo kutokana na yaliyotokea na hivyo tunahakikisha hali kama hiyo haitatokea tena”.

Paul Ryan mgombea mwenza wa Mitt Romney aliushambulia utawala wa Obama kwa kutompatia balozi wake usalama wa kutosha huko Benghazi. Alisema “Balozi wa Marekani mjini Paris anakikosi cha usalama kinachomlinda jee haijabidi kuwepo na kikosi kama hicho kumlinda balozi wao huko Libya?”.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema inaonekana wagombea hao wawili walitetea vyema sera za vyama vyao. naye Pius Macha, mchambuzi wa masuala ya kisiasa Minnesota anasema bwana Obama amepata msaada mkubwa katika kampeni yake kutokana na jinsi Joe Biden alivyojitetea.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:57 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mdahalo wa Wagombea hao wawili wa kiti cha Makamu Rais ulifanyika katika chuo kikuu cha Kentucky. Baada ya mdahalo huu wa Alhamis wachambuzi na waatalamu watafanya uchunguzi wao kuona nani ameshinda na hivyo nani ameweza kumsaidia mgombea wake kati ya Rais Obama na Romney. Hadi hivi sasa inavyo-onekana kufuatana na uchunguzi wa maoni mashindano ni makali kati ya Obama na Romney.
XS
SM
MD
LG