Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:36

Viongozi wa dunia wahudhuria maziko ya Atta Mills mjini Accra


wakazi wa Ghana wanakwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais John Atta Mills katika jengo la bunge mjini Accra, Ghana, Ogust 9, 2012.
wakazi wa Ghana wanakwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais John Atta Mills katika jengo la bunge mjini Accra, Ghana, Ogust 9, 2012.
Viongozi 18 wa Afrika na wawakilishi kutoka nchi mbali mbali za dunia waungana na maelfu ya Waghana kuhudhuria mazishi ya rais wa zamani John Atta Mills, aliyefariki Julai 24.

Bwana Mills aliyekua akiuguwa kwa muda mrefu na saratani ya koo, alifariki miezi mitano tu kabla ya kugombania mhula wa wake wa pili. Alikua kiongozi wa tatu wa Ghana aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia tangu kurudishwa tena mfumo wa vyama vingi nchini Ghana miaka ya 1990.

Atazikwa karibu na majengo ya serikali katika kasri la karne ya 17 lijulikanao kama Fort Christianborg, au Kasri la Osu.


Wachambuzi wanasema kifo chake kimewaunganisha wa Ghana nna kuwa mtihani mkubwa kwa mfumo wao wa kidemokrasia kwa kushuhudia mpito wa amani wa kisiasa. Makamu rais John Dramani Mahama aliapishwa saa chache baada ya kifo cha Bwana Mills.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa marekani Hillary Clinton alikuwa miongoni mwa wageni wa heshima walohudhuria mazishi hayo. Anakutana na Rais Mahama mjini Accra hii leo.
XS
SM
MD
LG