Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:32

Mauaji ya kikatili Syria


Serikali ya Syria inalaumu kile inachoita magaidi waliokuwa na silaha kwa mauaji ya kikatili ya zaidi ya raia.

Serikali ya Syria inalaumu kile inachoita magaidi waliokuwa na silaha kwa mauaji ya kikatili ya zaidi ya raia 108 siku ya Ijumaa karibu na mji wa Homs. Lakini mashahidi wengi wanasisitiza kuwa vikosi vinavyounga mkono serikali ndivyo vilifanya mauaji hayo ya kikatili. Maandamano yenye jazba juu ya mauaji ya raia yaliyofanyika Ijumaa huko Houla yanaendelea kote nchini Syria hiyo jana, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Damascus ambako vikosi vya uslama vilishambulia kwa risasi waandamanaji katika mtaa wa Midan. Msemaji wa wizara ya masuala ya nchi za nje wa Syria Jihad Makdissi aliwaambia waandishi habari kuwa jeshi la Syria halina lawama juu ya shambulizi la Ijumaa akisema wakulaumiwa ni magaidi waliokuw ana silaha. Mashambulizi hayo yalifanywa kwa saa tisa ambapo pamoja na mauaji, nyumba zilichomwa moto na mali kupora.

XS
SM
MD
LG