Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:52

Rais wa Jamhuri ya Congo aibuka mshindi tena

Rais wa Jamhuri ya Congo , Denis Sassou N'Guesso.
Rais wa Jamhuri ya Congo , Denis Sassou N'Guesso.

Matokeo rasmi yanaonyesha Guy Brice Pafair Kolelas akiwa wa pili kwa asilimia 15 akifatiwa na Jean Marie Michel Mokoko kwa nafasi ya 3 akiwa na asilimia 14 ya kura zilizopigwa.

Rais wa Jamhuri ya Congo, Denis Sassou Nguesso, ametangazwa kuwa mshindi baada ya uchaguzi wa Jumapili ambao upinzani umedai kujawa na dosari.

Waziri wa mambo ya ndani, Raymond Zephyrin Mboulou, ametangaza matokeo hayo kwenye televisheni ya kitaifa saa tisa na nusu asubuhi ya leo akisema kuwa Nguesso alijipatia asilimia 60 ya kura zilizopigwa.

Matokeo rasmi yanaonyesha Guy Brice Pafair Kolelas akiwa wa pili kwa asilimia 15 akifatiwa na Jean Marie Michel Mokoko kwa nafasi ya 3 akiwa na asilimia 14 ya kura zilizopigwa.

Wapinzani wote wawili wa rais Nguesso wamekataa kukubali matokeo hayo yalioanza kutolewa jumatano. Kwenye mahojiano na kituo cha radio cha France Internationale, Mokoko ameombwa kuundwa kwa kamati huru itakayotadhmini matokeo kutoka kita kituo cha kupigia kura

XS
SM
MD
LG