Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:55

Mateka wa Kenya warejea Mombasa


Manwari ya kimarekani USS Nicholas ikifanya doria kwenye pwani ya Somalia kuwasaka maharamia.
Manwari ya kimarekani USS Nicholas ikifanya doria kwenye pwani ya Somalia kuwasaka maharamia.

Wafanayakazi 39 raia wa Kenya na pamoja na wawili wa Korea Kusini na wawili wa China wailiwasili Mombasa Kenya kwa meli ya uvuvi ya Korea siku Jumanne.

Ilikuwa ni chereko, shangwe na vifijo katika bandari ya Mombasa baada ya ndugu za mateka hao kuwaona ndugu zao baada ya miezi mitano waliokaa huko Somalia.

Meli hiyo ya uvuvi inayomilikiwa na Korea Kusini yenye tani 241 iitwayo Keummi ilitekwa nyara mapema Oktoba ya 2010.

Ilipowasili kwenye bandari ya Mombasa walipokelewa na balozi wa Korea Kusini Lee Han-gon, jeshi la wanamaji wa Kenya na maafisa wengine wa serikali na mfanya biashara wa Korea Kusini Kim Jong Kyu ambae alikuwa akiwasiliana na maharamia hao.

Kabla ya kutoka kwenye meli hiyo walifanyiwa uchunguzi wa afya zao na walionekana kuchoka sana lakini hawakuonyesha ishara yeyote ya magonjwa mengine.

Maafisa wa Korea Kusini wanasema hakuna fidia yeyote iliyolipwa lakini ili waachiwe na mmoja wa mabaharia hao Daniel Odea anaeleza kuwa kapteni wa meli yao alikubaliana na maharamia wawasaidie kwenye kazi za kiharamia ambapo walijikuta bila kupenda wakishiriki katika zoezi la kuteka nyara meli nyingine kama vile York LPG iliyokuwa ikitoka Mombasa.

Wanasema waliteka nyara meli nyingine ambayo walifikishwa mpaka Usheli sheli na kuteka meli ya Iran na wameacha meli 15 katika pwani ya Somalia na maharamia.

XS
SM
MD
LG