Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:13

Mashua yazama Ziwa Victoria, watu kadhaa wafariki.


Ziwa Victoria
Ziwa Victoria

Mamlaka nchini Uganda zinasema zaidi ya watu kumi wamekufa wakati mashua waliyokuwa wakisafiria ilipozama katika ziwa Victoria huku kukiwa na upepo mkali.

Mamlaka nchini Uganda zinasema zaidi ya watu kumi wamekufa wakati mashua waliyokuwa wakisafiria ilipozama katika ziwa Victoria huku kukiwa na upepo mkali.

Msemaji wa jeshi la polisi, Uganda, Vincent Ssekamatte amesema wafanyakazi wa uokozi waliokoa watu wanne kutoka majini wakiwa hawajitambui na walikimbizwa hospitali ambako walilazwa.

Kuna ripoti za utatanishi juu ya kiasi cha watu waliokuwamo ndani ya boti hiyo . Shirika la habari la Ufaransa limemnukuu msemaji wa jeshi la polisi akisema kuwa inasadikiwa takriban watu 60 wanaweza kuwa walikuwamo ndani.

Boti hiyo ilikuwa inasafirisha abiria na samaki kutoka katika kisiwa kwenye ziwa Victoria na ilikuwa inatarajiwa kwenda karibu na Entebe, kusini mwa mji mkuu wa Kampala. Mamlaka zinasema ilikuwa imejaa watu kupita kiasi tatizo la mara kwa mara la wasafirishaji katika maji ya Afrika.

Mamia ya watu wamekufa kutokana na ajali kama hizo katika ziwa Victoria miaka ya hivi karibuni. Ajali iliyokuwa na maafa makubwa ya vifo ilitokea Mei mwaka 1996 wakati meli ilipozama ikiwa njiani kuelekea Mwanza, Tanzania na kuuwa takriban watu 800 waliokuwemo ndani.

XS
SM
MD
LG