Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:39

Mashambulizi ya Boko Haram ni ya ukatili dhidi ya binadamu


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, akiwa nchini Bulgaria, Januari, Jan. 15, 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, akiwa nchini Bulgaria, Januari, Jan. 15, 2015.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amesema mashambulizi ya hivi karibuni ya wanamgambo wa Boko Haram, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria yalikuwa ya ukatili dhidi ya binadamu.

Bwana Kerry alisema hayo wakati wa ziara yake ya nchini Bulgaria, ikiwa ni siku moja baada ya shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International, kutoa picha za setelaiti zikionyesha uharibifu mkubwa uliofanywa na wapiganaji wa Boko Haram katika miji miwili.

Bwana Kerry amesema Boko Haram ni moja ya vikundi vibaya na vya kigaidi duniani.

Kundi hilo la kigaidi, limekuwa likifanya mashambulizi mfululizo nchini Nigeria, na Cameroun, huku likisababisha raia kadhaa kuyakimbia makazi yao.

XS
SM
MD
LG