Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:40

Wanajeshi 5 wauliwa Sudan Kusini


Maafisa wa jeshi la Sudan Kusini wanaeleza kwamba wanajeshi 5 wa Serikali ya Sudan Kusini waliuawa jana Alhamisi wakati wa mashambuliano ya bunduki kati ya makundi yenye silaha yanayohasimiana katika mji mkuu wa Juba.

Wakati huo huo ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo imeeleza kushambuliwa kwa afisa wake wa cheo cha juu wakati hali ya wasi wasi inaongezeka juu ya uwezekano wa kurudi tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan Kusini.

Mashambuliano hayo yalitokea siku mbili kabla ya maadhimisho ya mwaka wa tano tangu nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka kwa Sudan.

Msemaji wa jeshi la serikali, Lul Rusi Kosng, alisema kuwa msafara wa wanajeshi wa makamu rais wa kwanza, Rieck Machar, walifyetulia risasi kituo cha ukaguzi mjini Juba kinachosimamiwa na wanajeshi watiifu na Rais Salva Kiir na kwamba wanajeshi watano wa kikosi cha wanajeshi watiifu na rais.

XS
SM
MD
LG