Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:32

Marekani yaadhimisha “Black History Month” Kenya


Baadhi ya bendi za muziki zikiimbimba kusherehekea historia ya watu weusi katika ikulu ya Marekani February 21, 2012.
Baadhi ya bendi za muziki zikiimbimba kusherehekea historia ya watu weusi katika ikulu ya Marekani February 21, 2012.

Maonyesho hayo tayari yamezinduliwa katika makavazi ya Malindi au Museum, na katika muda wa wiki mbili yaatelekezwa mji wa Gede na hatimaye Mombasa.

Ubalozi wa Marekani nchini Kenya umetenga siku 14 za maonyesho maalum katika mkoa wa Pwani, kuadhimisha sherehe za “Black History Month”.

Taarifa kutoka ubalozi huo zinasema kutakuwa na hafla tofauti katika miji ya kitalii huko Mombasa na Malindi, ikiwa ni pamoja na kuhusu Uislamu nchini Marekani.

Pia serikali ya Marekani imezindua mpango wa maonyesho ya picha hapa mkoani Pwani, kuhusu hali ya Uislamu nchini Amerika.

Eneo hilo lina waislamu wengi zaidi nchini Kenya, na huu unaonekana ni wakati muafaka wa kuwaeleza hayo –kutokana na sherehe hizi za “Black History Month” – Mwezi wa Historia ya Watu Weusi".

Maonyesho hayo tayari yamezinduliwa katika makavazi ya Malindi au Museums, na katika muda wa wiki mbili yaatelekezwa mji wa Gede na hatimaye Mombasa.

Dhamira kuu ni kusherehekea ushirikiano wa Wamarekani weusi tangu ukoloni, sherehe ambayo hufanyika mwezi wa pili kila mwaka.

Lakini pia Marekani ina lengo fulani katika ushirikiano huo.

Afisa wa habari katika ubalozi wa America hapa Kenya -Henry Mendelesohn amesema huu ni muda mwafaka kwa kizazi cha sasa kujifunza mengi kuhusu Marekani, na pia kuondoa dhana kwamba nchi hiyo haiungi mkono Uislamu.

Maidhui ya mwaka huu wa 2012 ya Black History Month ni Wanawake Weusi katika Utamaduni na Historia ya Amerika.

XS
SM
MD
LG