Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:53

Marekani yatangaza marufuku ya uuzaji wa ndani wa pembe za ndovu


John Kerry, waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
John Kerry, waziri wa mambo ya nje wa Marekani.

Serikali ya Marekani imetangaza marufuku ya uuzaji wa ndani wa pembe za ndovu hatua inayolenga kuwalinda wanyama walio hatarini kumalizwa.

Awali pembe za ndovu zinaweza kuuzwa kama zililetwa Marekani kabla tembo hawajaorodheshwa kama wanyama waliopo hatarini kumalizwa au kama kulikuwa na hati inayotoa maelezo tembo alikufa kwa sababu za kawaida.

Kanuni mpya inadhibiti uuzaji wa bidhaa za mnyama huyo kama vile sanamu za pembe za ndovu au vinyago na vitu kama vifaa vya muziki vilivyotengenezwa kwa kutumia chini ya gram 200 ya pembe za ndovu.

Bidhaa zilizotengenezwa na pembe za ndovu huko Hong Kong.
Bidhaa zilizotengenezwa na pembe za ndovu huko Hong Kong.

Tangazo hilo limekuja siku chache kabla ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry na waziri wa fedha Jack Lew kutembelea China moja ya mataifa kadhaa ya Asia mahala ambako mahitaji ya pembe za ndovu bado ni makubwa sana. Mahitaji hayo yamewachochea majangili ambao wanawauwa tembo wa kiafrika kwa ajili ya pembe zao.

San Ashe mkurugenzi wa idara ya huduma za uvuvi na wanyama pori nchini Marekani alisema maafisa sasa wanaweza kusema Rais Barack Obama ametimiza ahadi yake kukaribia kumaliza uuzaji wa ndani wa pembe za ndovu na anaweza kuwaomba viongozi wa China kufanya vivyo hivyo.

XS
SM
MD
LG