Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 13:24

Marekani yasheherekea miaka 236 ya uhuru


Members of Kosovo ballet perform during an event to raise awareness on breast cancer in Pristina. 
Members of Kosovo ballet perform during an event to raise awareness on breast cancer in Pristina. 

Rais Barack Obama ataongoza sherehe za Julai 4 kwa gwaride maalumu la jeshi huko White House na michezo mingine

Rais wa Marekani Barack Obama, Jumatano ataungana na wamarekani kote nchini kusheherekea siku ya uhuru wa Marekani – Julai 4. Rais Obama ataongoza sherehe huko White House ambapo kutakuwa na gwaride la jeshi, likifuatiwa na matukio ya nyama choma, michezo na burudani itakayotolewa na Marine Band.

Mamilioni ya Wamarekani katika miji na vitongoji vyake wanasheherekea siku hii kwa matukio mbali mbali ikiwemo gwaride, kuangalia ufyatuaji wa fataki, nyama choma, burudani na mkusanyiko wa familia na marafiki kutoka sehemu mbali mbali kote nchini.

Mjini Washington, maelfu ya watu hukusanyika katika eneo linaloitwa National Mall ambapo huangalia burudani kupitia televisheni na baadae fataki zinazofyatuliwa kitaalam.

Fataki pia zitafyatuliwa hewani usiku kwenye maeneo ya mapigano kutoka vita ya mwaka 1812 na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika karne ya 19. Matukio kama haya pia yatafanyika katika majimbo ya Philadelphia, Annapolis, Maryland na New York City.

XS
SM
MD
LG