Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:12

Marekani yamuunga mkono Hadi wa Yemen


Rais wa Yemen anayetakubalika na Marekani Abed Rabbo Mansour Hadi.
Rais wa Yemen anayetakubalika na Marekani Abed Rabbo Mansour Hadi.

Marekani imetangaza kwamba inamuunga mkono bwana Abed Rabbo Mansour Hadi, wa Yemen, kama kiongozi wa haki wa nchi hiyo, kupitia mjuumbe maalum anaetembelea nchi hiyo.

Tangazo hilo lilitolewa wakati wa ziara ya balozi wa Marekani, Matthew Tueller, katika mji wa kusini wa Yemen, wa Aden, ambako bwana Hadi, ameweka makazi yake baada ya waasi wa Houthi kumuweka kuzuizini nyumbani kwake katika mji mkuu wa Sanaa na kumlazimisha kujiuzulu.

Huo ulikuwa ni mkutano wao wa kwanza wa hadharani toka Washington, ilipofunga ubalozi wake mwezi uliopita mjini Sanaa.

Wanamgambo walichukua udhibiti wa mji mkuu ambao ulikumbwa na ghasia kwa miezi kadhaa kabla ya kundi la wa Houthi kujitangazia mamlaka mwezi Januari.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Jen Psaki, amesema Marekani, itaendelea kuwa karibu na Wayemen, na jumuiya ya kimataifa kusaidia mpito wa kisiasa wa Yemen, ambao unaongozwa na mikataba mbalimbali iliyosimiamiwa na jumuia ya kimataifa.

XS
SM
MD
LG