Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:28

Marekani yaikatia Rwanda msaada wa kijeshi


Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakiwa katika doria ndani ya DRC
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakiwa katika doria ndani ya DRC

Washington inasema itazuia msaada wa dolla laki mbili ambao ungesaidia idara ya mafunzo ya kijeshi Rwanda

Marekani imekata msaada wake wa kijeshi kwa Rwanda kutokana na wasiwasi kuwa serikali ya Kigali inaunga mkono waasi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema ina ushahidi kuwa Rwanda inasaidia makundi ya waasi wa Congo, ikiwa ni pamoja na kundi la M23. Imesema itazuia msaada wa dolla 200,000 ambazo zilikuwa ziende katika idara ya mafunzo ya kijeshi ya Rwanda. Serikali ya Rwanda mara kwa mara imekanusha kusaidia waasi wa DRC.

Hatua ya Washington imekuja wiki moja baada ya marais wa Rwanda na DRC kukubaliana kuhusu kupelekwa kwa jeshi la kimataifa kupambana na waasi mashariki mwa Congo na kulinda doria katika mpaka unaounganisha nchi hizo.

Majeshi ya Congo yamejaribu kwa miaka kadha, bila mafanikio, kuzima makundi ya waasi katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa madini.

Kundi la M23 linaundwa na wanajeshi wa zamani inaoaminika kuwa ni wafuasi wa Bosco Ntaganda, mbabe wa kivita anayetafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa madai ya uhalifu wa wakati wa vita.

XS
SM
MD
LG