Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 05:26

Marekani yafurahishwa na juhudi za mazungumzo ya amani ya Arusha


Mpatanishi wa mazungumzo ya amani huko Burundi, Rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa
Mpatanishi wa mazungumzo ya amani huko Burundi, Rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa

Serikali ya Marekani inasema imetiwa moyo na mashauriano ya karibuni ya mjini Arusha, Tanzania na maendeleo katika majadiliano mapana miongoni mwa wadau kupata suluhisho la amani kwa mzozo wa Burundi.

Katika taarifa yake naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Mareknai, Mark Toner alisema wanapongeza juhudi za rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa katika kufanikisha mashauriano na kuahidi kuhakikisha kuwa mkutano ya baadaye utajumuisha wahusika wote.

Naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Mark Toner.
Naibu msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Mark Toner.

Bwana Toner alisema wamefurahishwa na hali ya uharaka iliyoonyeshwa na washirika katika kupanga tarehe kwa hatua zijazo. Ni muhimu sana kwa wadau wote kuwakilishwa katika mashauriano ikiwemo viongozi wa sasa na wa zamani wa upinzani pamoja na vyama vya kiraia ili kuweka mazingira bora ya majadiliano chanya, pande zote alisema bwana Toner lazima ziache aina yoyote ya ghasia na serikali ni vyema iache vitendo vyote vya mateso na kuwatia ndani wanasiasa.

Marekani imesimama tayari kuunga mkono utaratibu wa amani pamoja na kuweka vikwazo vya ziada vinavyohitajika dhidi ya watu wanaohusikana na ukiukaji wa haki za binadamu.

XS
SM
MD
LG