Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:26

Marekani:Wabunge wagawanyika kuhusu Syria


Waandamanaji wanaopinga serikali ya Syria.
Waandamanaji wanaopinga serikali ya Syria.
Wabunge wa Marekani bado hawajafikia maelewano kupiga kura juu ya kuunga mkono mashambulizi ya kijeshi dhidi ya serikali ya rais Bashar al-Assad au kupinga. Baadhi yao walizungumza baada ya kupokea taarifa kuhusu Syria kutoka kwa maafisa wa Marekani Jumapili.

Wanatarajiwa kurejea bungeni Septemba 9 lakini baadhi yao walihudhuria kikao Jumapili jijini Washington ambapo maafisa waliwaelezea mpango wa kuingilia kati mzozo wa Syria. Baada ya kikao hicho baadhi yao walisema wanaamini silaha za kemikali zilitumiwa lakini kungali na maswali kadha.

Mbunge wa chama cha Demokrat Janice Hahn, anauliza ikiwa hii ni sababu ya kwenda vitani. Kuna lengo gani la kwenda vitani? Je tunampa idhini ya aina gani rais? aliuliza mbunge huyo.

Hahn anasema Marekani haipaswi kuingia vitani peke yake. Naye mbunge wa chama cha Republican Scott Rigell alisifu uamuzi wa rais Obama wa kuomba idhini ya wabunge. Lakini akasema kwa sasa jibu litakuwa ’hapana’. Alisema hataunga mkono kura hiyo kwa sababu haijabainika wazi lengo la kuingia vitani huko Syria ni lipi. Mbunge wa chama cha democrat Sandy Levin anaunga mkono majeshi ya Marekani kuingilia kati mzozo wa Syria. Anasema ana imani kuwa wabunge wataunga mkono kura hiyo kwa sababu wasipofanya hivyo watakuwa wanapeleka ujumbe usio sahihi.

Jumamosi rais Obama alisema hahitaji idhini ya bunge kushambulia, lakini anahitaji uungaji mkono wa wawakilishi wa taifa waliopo Washington.

Jumapili waziri wa mambo ya nje John Kerry alizungumza kwenye vituo kadha vya televisheni akieleza kile ambacho utawala wa Obama umefahamu kutoka na mashambulizi ya mwezi jana dhidi ya raia mjini Damascus na maeneo jirani. Kerry alisema Marekani isipochukua hatua itakuwa inampa nafasi dikteta katili kuendelea kutumia gesi ya sumu dhidi ya watu wake.
XS
SM
MD
LG