Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:38

Marekani yazitaka pande husika Sudan Kusini kutekeleza makubaliano ya amani


Wanajeshi wa upande wa uasi huko Sudan Kusini wakionyesha silaha zao kwenye kambi ya jeshi katika mji mkuu Juba, Aprili 7, 2016.
Wanajeshi wa upande wa uasi huko Sudan Kusini wakionyesha silaha zao kwenye kambi ya jeshi katika mji mkuu Juba, Aprili 7, 2016.

Marekani inapanga kutochuka nafasi muhimu katika mashauriano ya amani kati ya serikali ya Sudan Kusini na viongozi wa waasi kufuatia kwa pande zote kushindwa kutekeleza mkataba wa kuunda serikali ya mpito.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, John Kirby, alisema katika taarifa yake kwamba siku ya Jumamosi serikali ya Sudan Kusini ilikataa kutoa kibali cha kutua kwa ndege iliyokuwa ikimsafirisha kiongozi wa upinzani Riek Machar, kwa sababu kiongozi huyo wa waasi "aliomba kiholela" kuingia na silaha na wanajeshi kinyume na vile pande hizo mbili zilivyokubaliana hapo awali.

Kirby anasema kutokana na hatua zilizochukuliwa na pande zote mbili ya kuzuia au kuchelewesha kurudi kwake, hivi sasa ni juu ya pande husika kuchukua majukumu ya kufanikisha kurejea kwa Riek Machar mjini Juba ili kuunda serikali ya mpito na kuonyesha kwamba wana nia ya dhati ya kw amani.

XS
SM
MD
LG