Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:45

Marekani yailaumu Rwanda.


Mwakilishi wa Marekani katika eneo la maziwa makuu Tom Perriello akizungumza na waandishi wa habari.
Mwakilishi wa Marekani katika eneo la maziwa makuu Tom Perriello akizungumza na waandishi wa habari.

Wanadiplomasia wa juu wawili wa Marekani wameilaumu Rwanda kwa kupelekea hali ya kutokuwa na uthabiti Burundi ambako ghasia za kisiasa zimeacha mamia kupoteza maisha yao.

Naibu waziri wa mambo ya nje anayeshughulikia masuala ya Afrika Linda Thomas Greenfield alizungumzia wasi wasi wake kwenye kamati ya mambo ya nje ya baraza la seneti .Alikariri idadi kubwa ya ripoti za maafisa wa Marekani walioko barani Afrika.

“Tumeeleza wasi wasi wetu kwa serikali ya Rwanda na kuwaomba wachukue nafasi yenye tija na wasifanye chochote cha kuondoa uthabiti nchini Burundi Thomas Greenfield aliwaambia waandishi wa habari.

Mwakilishi mwingine wa bara la Afrika katika eneo la maziwa makuu Tom Perriello amesema taarifa za kuaminika kwamba maafisa wa Rwanda wanawapa mafunzo wakimbizi wa Burundi ili kushirikiana na upinzani wa Burundi.

Perriello amesema watoto ni kati ya wakimbizi wanaofundishwa kupambana.

XS
SM
MD
LG