Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:51

Malawi yazindua kampeni ya kuwalinda walemavu wa ngozi


Watu wenye ulemavu wa ngozi
Watu wenye ulemavu wa ngozi

Takriban watu 17 wenye ulemavu wa ngozi wameuwawa nchini Malawi katika kipindi cha miaka 2 ilopita

Sheria thabiti zinahitajika kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi- albino nchini Malawi, kutokana na mashambulizi yasiyoeleweka. Kwa mujibu wa watetezi wa haki za kiraia ambao wameandamana hadi kwenye bunge la nchi hiyo. Umoja wa mataifa umeonya mwezi uliopita kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Malawi wako katika hatari ya kuangamizwa kabisa kutokana na ongezeko la mauwaji na mashambulizi ya kuwakata viungo.

Watu mia kadhaa walishiriki katika maandamano hadi kwenye bunge mjini Lilongwe. Moja ya mabango yao limeandikwa “amkeni wabunge wetu”.

Edward Chileka Banda ni mwenyekiti wa maandalizi ya maandamano hayo.

Banda anasema, kuwasilishwa kwa malalamiko hayo kwa bunge kunaadhimisha nia yetu ya dhati kama raia na makundi ya kiraia kudai kusitishwa mara moja na kumaliza mauwaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Malalmiko hayo yanataka watu wanaoshambulia watu wenye ulemavu wa ngozi kupewa hukumu ya kifungo cha maisha gerezani.

Mbunge Ester Jailosi Jolobala alipokea barua ya malalamiko hayo kwa niaba ya spika wa bunge. Anasema wabunge watachukuwa hatua ya haraka.

Bi Jolobala anasema kuwa inakera sana unapoona wahalifu wakiachiliwa aidha kutokana na kulipa dhamana au kutokana na adhabu ambazo si kali sana. Hii inazidisha hofu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi hapa Malawi.

Takriban watu 17 wenye ulemavu wa ngozi wameuwawa nchini Malawi katika kipindi cha miaka 2 ilopita. Wahalifu wachache wameweza kukamatwa.

Rais wa shirikisho la watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Malawi, Boniface Massah, anasema kwa mda mrefu Malawi imekuwa ikitoa maneno matupu tu katika kuzungumzia juu ya mashambulizi.

Bw. Massa anasema,kasi ya kutathmini sharia lazima izidishwe. Na kunapaswa kuwa na raslimali za kushughulikia utaratibu huo.

Watu wenye ulemavu wa ngozi wanalengwa nchini Malawi na katika maeneo mengine ya Afrika kwa sababu ya Imani potofu ya kuwa dawa zinazotengenezwa kutokana na viungo vyao vya mwili kuwa vitaleta utajiri na bahati nzuri.

Malawi imetenga wiki hii kwa kuongeza uwelevu zaidi juu ya suala hilo. Ligi kuu ya taifa ilianza kampeni yake ya Game Over, inayolenga kuongeza uwelevu juu ya uovu wa mashambulizi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Ligi hiyo imewaalika watu wenye ulemavu wa ngozi kwenye mechi maalum na kuweka mabango kote kwenye uwanja wa mpira yanayokosoa mashambulizi .

XS
SM
MD
LG