Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:38

Mutharika Aapishwa Urais Malawi


Bendera ya Palestina yapeperuka kwenye uwanja wa Umoja wa Mataiufa
Bendera ya Palestina yapeperuka kwenye uwanja wa Umoja wa Mataiufa

Peter Mutharika ashinda uchaguzi wa Malawi kwa kupata asilimia 36 ya kura na kumwondoa madarakani rais wa kwanza mwanamke nchini humo Joyce Banda

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Progressive nchini Malawi, Peter Mutharika, ameapishwa leo kama rais wa nchi hiyo. Bw Mutharika mwenye umri wa miaka 74 alisema katika hotuba fupi kuwa kazi yake kubwa itakuwa kuwaunganisha wamalawi baada ya mvutano wa muda mrefu katika maswala ya uchaguzi.

Ametoa wito kwa washindani wake kuungana naye katika kujenga taifa. Maafisa uchaguzi Ijumaa walimtangaza Mutharika kama mshindi wa uchaguzi wa wiki iliyopita uliokuwa na utata na kumshinda rais aliyekuwa madarakani Joyce Banda.

Tume ya uchaguzi ya Malawi ilitangaza matokeo hayo Blantyre, saa kadha baada ya waandamanaji waliokuwa wakidai hesabu mpya ya kura kupambana na polisi katika mji wa Mangochi – kusini mwa nchi. Inaripotiwa kuwa mtu mmoja alifariki katika ghasia hizo.

Hesabu ya mwisho inayonyesha kuwa Bw Muthariki alipata kiasi cha asilimia 36 ya kura, na chama cha Malawi Congress cha Lazrous Chakwera kilipata asilimia 29. Rais Banda alimaliza na asilimia 20 tu ya kura. Bw Mutharika ni kaka wa rais wa zamani marehenu Bingu wa Mutharika.
XS
SM
MD
LG