Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 10:56

Malawi yapata chakula cha kutosha


Rais wa Malawi Peter Mutharika amesema nchi yake hivi sasa imepata chakula cha kutosha kulisha nusu ya idadi ya watu nchini humo ambao wanahitaji msaada wa chakula.

Akilihutubia taifa kwa mara ya pili tangu mwezi Mei, amesema anafahamu maumivu wanayokabiliana nayo wananchi wengi.

Pia amesema anaelewa kwamba kuna hali ya kutokuwa na uvumilivu wa kuondokana na changamoto zinazowakabili kwasababu taifa linaathiriwa na umaskini wa miaka mingi.

Malawi ina tatizo kubwa la ukosefu wa chakula kuwahi kutokea kwa muongo mzima.

Watalaamu wanasema hali hii kwa kiasi kikubwa imetokana na hali ya hewa ya El Nino ambayo imesababisha ukame na mafuriko ambayo yameathiri mazao kwa miaka miwili iliyopita.

Ripoti ya karibuni kutoka kamati ya tathmini imeonyesha kwamba wananchi milioni 6.7 wa Malawi wana shida kubwa ya msaada wa chakula.

Idadi hiyo ni sawa na nusu ya watu wote nchini humo.

XS
SM
MD
LG