Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:24

Makundi yamsihi Obama kubadilisha sera za kibaguzi


Mamia ya makundi ya kutetea haki za kiraia yamemuomba rais wa marekani Barack Obama kuivunja program ambayo iliwahi kutumika kuandikisha wageni kutoka nchi kadhaa za kiislamu.

Programu hiyo ilikuwa ni katika juhudi za kuuzuia utawala ujao wa Donald Trump kufufua utaratibu huo.

Katika barua yao kwa Obama ambayo imebandikwa katika mtandao Jumanne, taasisi 198 za ndani na za kitaifa za Marekani zimetaka hatua za kiutendaji zichukuliwe haraka.

Hatua hizo ni kubatilitisha mfumo wa usalama wa taifa wa kuandikisha wageni wanaoingia na kutoka ambao unajulikana kama NSEERS.

NSEERS ilikuwa ni sera ya kibaguzi ambayo ilienda kinyume na misingi ya Marekani ya haki na usawa kwa wote.

Barua ya kundi hilo imeandika na kuongezea kwamba ulikuwa haikuwa nyenzo muafaka kukabiliana na ugaidi, na kupelekea athari nyingi kwa watu binafsi ambao waliathiriwa moja kwa moja na kuvuruga uhusiano na jamii za wahamiaji.

XS
SM
MD
LG