Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 10:04

Majeshi ya Libya yawafurusha tena wapinzani


Mpiganaji wa upinzani aliyejeruhiwa anatibiwa katika hospitali mjini Adabiyah baada ya kufikishwa huko kutoka Ras Lanuf, Mrachi 30, 2011
Mpiganaji wa upinzani aliyejeruhiwa anatibiwa katika hospitali mjini Adabiyah baada ya kufikishwa huko kutoka Ras Lanuf, Mrachi 30, 2011

Wapiganaji wa Libya walifurushwa kuelekea mashariki baada ya majeshi ya Gadhafi kuchukuwa tena udhibiti wa mji wa mafuta wa Ras Lanuf

Wanajeshi wa serikali ya kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi waliwafurusha wapiganaji wa upinzani kutoka mji huo muhimu wa mafuta baada ya kuchukua tena udhibiti wake siku ya Jumatano.

Ripoti za vyombo vya habari kutoka Ras Lanuf zinaeleza kwamba, wapiganaji walikuwa wanarudi nyuma kufuatia mapigano makali ya roketi.

Ripoti zinaeleza idadi kubwa ya wapiganaji walikimbia wakitumia malori madogo na hivyo kupoteza tena udhibiti wa maeneo walokombowa tangu mwishoni mwa wiki walipokuwa wanaelekea upande wa magharibi.

Hali katika uwanja wa mapigano ilianza kubadilika Jumanne usiku pale wanajeshi wa Libya walipoanza kuwashambulia wapiganaji kwa mizinga na roketi na kusababisha hofu kubwa katika mji wa Ras Lanuf.

XS
SM
MD
LG