Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:34

Mazungumzo ya kutafuta amani Burundi yaanza


Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga.
Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga.

Mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa Burundi yameanza rasmi Jumatatu mjini Kampala Uganda chini ya usimamizi wa mpatanishi rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na wawakilishi wa serikali ya Burundi, wapinzani wa utawala wa rais Pierre Nkurunzinza , wawakilishi wa jamii za kiraia na wawakilishi kutoka nchi za Afrika Mashariki.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:21 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kikao cha Jumatatu kilikuwa ni uzinduzi wa jitihada mpya za kuanzisha na kusukuma mazungumzo ya amani kati ya warundi na majirani zao na hasa jumuiya ya Afrika Mashariki. Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga ameiambia Sauti ya Amerika kwamba waliona kuna umuhimu wa kuwasaidia na kuwahimiza kuanzisha utaratibu wa kuzungumza baina yao.

XS
SM
MD
LG